Maswali ya Mara kwa Mara
Majibu mafupi kuhusu huduma, maombi, KYC, malipo na usalama.
Ninaanzaje kuomba huduma?
Fungua akaunti kwenye portal.fkf.co.tz, kamilisha KYC na uchague huduma inayopatikana. Maombi rasmi hayatumiwi kupitia WhatsApp.
Je, kiwango cha riba na ada ni kiasi gani?
Kiwango halisi hutegemea bidhaa na tathmini. FKF itakupa gharama na ratiba kwa maandishi kabla ya mkataba. Usitumie makadirio ya website kama ofa rasmi.
Kwa nini KYC inahitajika?
KYC husaidia kuthibitisha utambulisho, mawasiliano, anwani na nyaraka zinazohitajika kabla ya maombi kutathminiwa.
Nitajuaje kama malipo yangu yamepokelewa?
Angalia hali ya malipo na risiti ndani ya portal. Unaweza pia kutumia ukurasa wa Uhakiki wa Risiti baada ya API kuunganishwa.
FKF itaomba PIN au OTP yangu?
Hapana. Usimpe mtu PIN, OTP, nenosiri au taarifa kamili za kadi, hata akijitambulisha kama mfanyakazi wa FKF.
Naweza kupata msaada kupitia WhatsApp?
Ndiyo, AMINA atakufikisha kwenye WhatsApp rasmi kwa maelezo ya kawaida. Usitume nyaraka nyeti au siri za akaunti kupitia WhatsApp.
Website na portal vina tofauti gani?
fkf.co.tz ni website ya taarifa za umma. portal.fkf.co.tz ni eneo salama la akaunti, KYC, maombi, malipo na risiti za mteja.